Mdahalo wa Afya ya Jamii
AFYA YETU, WAJIBU WETU
Je, unajua jinsi gani mafuta mabaya ya Trans Fats (TFAs) yanavyoathiri afya yako ya kila siku na kuleta mzigo mkubwa wa kiuchumi kwa Taifa letu?
Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu kushiriki katika mdahalo wetu wa afya ya jamii utakaokuwa mubashara (LIVE HEALTH TALK). Tutajadili, tutajifunza, na tutashirikiana kwa mustakabali wa afya bora kwa wote.
MADA: Madhara ya Trans fat acid kwa Afya ya Jamii na Uchumi wa Taifa
TAREHE: 12 Juni 2026, Ijumaa
MUDA: Saa 9:00 – 10:30 Mchana
MAHALI: Mkutano Mtandao kupitia Zoom.
Huu sio mjadala wa kukosa. Kushiriki kwako ni hatua kubwa kuelekea mabadiliko chanya ya sera na mifumo ya afya nchini kwetu. Wahi nafasi yako na ujisajili mapema sana kwani mjadala huu utakuwa na tija na mafunzo makubwa.
JISAJILI HAPA: https://bit.ly/4ohBN8c
(Au skani QR Code iliyopo kwenye bango letu la picha kujiunga rasmi).
#MjadalaWaAfya
#TransFatFreeTZ
#AfyaYetuWajibukWetu
hashtag#HakiHainaJinsia